Thursday 12 January 2017

Faiza Ally-Ukimwi ni maradhi tu kama mengine yote Mwisho wa siku hakuna alie piga goti akaomba

Image result for faiza ally instagram

faizaally_Naandika hii msg kwa ajili ya wagonjwa wa ukimwi wote duniani...imekua kawaida sana kutukanwa,kunyanyapaliwa,kusemwa mpaka kufikia kuona kwamba ugonjwa wa ukimwi ni aibu kubwa sana , na hii imesababisha watu wafiche maradhi kwa ajili ya kuogopa kashfa kama hizo! Pia imesababisha wagonjwa kuwa wakatili na kuugawa hovyo ili kukomoana.


Msg Yangu kwa waathirika wa ukimwi ni kama hivi.kuna walio pata kwa kuletea na mke au mume,kuna aliepata kupitia ncha kali au njia zingine ambazo zinaweza kuambukiza,kuna alie zaliwa nao na kuna alie utafuta kwa njia ya umalaya ... tukija kwa hao waliopata kwa njia za kuletewa au kwa bahati mbaya sio makosa yenu! Hata huyu alie pata kwa njia ya umalaya pia usimjaji sana maana hukupita alipo pita so far kwa ninavvyo jua Malaya wengi wako makini sana maana hata wanao nunua wana waogopa! mwisho wa siku wote ni wagonjwa ! Naomba nikwanbie ndugu Yangu wewe ulio athirika kuhusu ugonjwa wako! Kwanza kabisa unapo pata ukimwi unatakiwa kupokea ,kukubali na kushukuru MUNGU... baada ya hapo nikujitibu,kuwa makini ktk kuwapa wengine maana kuna athari pia za kuongeza virusi kupitia kungine unaweza ukahisi una sambaza kumbe unajiongezea! Lkn kikubwa zaidi angalia maradhi mengine tofauti ambao ni hatari kushinda ukimwi ndio utaona kwamba ni bora umepata ukimwi kulipo ungepata maradhi yanayo kuondoa duniani kwa dakika na kwa upande mngine angalia walemavu wasio jiweza kwa chochote hapa ndio utakapo ona ni bora maradhi yako ya ukimwi kuliko mengine ..malaria,kansa,kipindupindu haya ni maradhi hatari sana limonia na mengine mengi mno...yana kuondoa fasta sana ! So wewe mwenye ukimwi Leo maneno yawalimwengu yasikutishe kunywa dawa zako kwa amani na uendelee na maisha yako tena ikibidi kuwa huru! Ukimwi ni ugonjwa ambao unaishi,unazaa,unafanya kazi,unaolewa unaendelea na kila kitu na ratiba zote za maisha! Ukimwi usiku katishe tamaa ya kurudisha maisha yako nyuma kamwe! Ukimwi ni maradhi mwisho wa siku hakuna alie piga goti akaomba ni maradhi tu kama mengine yote ! Na yanaweza kumpata yoyote .... amani iwepo kwenye maisha yenu! Mungu ametoa mitihani kwa namna Nyingi sana huenda ukimwi ndio mtihani wako lkn kuna wenye mitihani mikubwa kushinda ukimwi

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!