Friday 8 July 2016

Beyonce alaani mauaji ya Wamarekani weusi

BeyonceImage copyrightREUTERS
Image caption''Sote tuna uwezo wa kuonyesha hasira zetu kivitendo'' alisema Beyonce
Mwanamuziki maarufu wa Marekani Beyonce amewataka wamarekani kufikikisha hasira na mkanganyiko kwa wanasiasa na wabunge wao kufuatia mauaji ya kibaguzi dhidi ya wamarekani weusi.


Watu maarufu nchini Marekani wamekua wakielezea hisia zao kuhusu kisa cha hivi karibuni ambapo polisi walionekana wakimpiga risasi mwanaume mweusi wa kimarekani.
Beyonce amesema ''sote tuna uwezo wa kuonyesha hasira zetu kwa vitendo'', akiwataka waMarekani kuwasiliana na wanasiasa wao wilayani na kudai haki ya kijamii na mabadiliko ya kisheria.
BeyonceImage copyrightGETTY
Image captionBeyonce alitulia kimya muda wa dakika moja kuwakumbuka wamarekani wawili weusi waliouawa wakati wa onyesho lake mjini Glasglow
Beyonce alitulia kimya kwa muda wa dakika moja wakati wa onyesho lake mjini Glasglow jana usiku kuwakumbuka wamarekani wawili waliouawa kwa kupigwa risasi, na kuweka majina yao Alton Sterling na Philando Castile kwenye screen kubwa huku akitoa wito wa kumalizika kwa ''vita dhidi ya walio wachache'' nchini Marekani
Beyonce na Jay ZImage copyrightGETTY
Image captionMumewe Beyonce Jay Z (pichani kulia) ametoa wimbo kuhusu mauaji ya risasi nchini Marekani
Mumewe Beyonce Jay Z ametoa wimbo mpya kuhusu ufyatuaji risasi. Katika wimbo wake wenye miondoko ya rap Jay Z anahoji kwanini Marekani haibadili sheria yake kuhusu silaha?.
Jumanne picha nyingine ya video ilijitokeza ambapo polisi wawili wa kizungu walionekana wakimsukuma chini na kumpiga risasi Alton Sterling mjini Louisiana.
 Alton Sterling Image copyrightAFP
Image captionAlton Sterling mmoja wa wamarekani weusi waliouawa kwa kupigwa risasi na polisi.
Siku iliofuatia mkanda mwingine wa video uliorekodiwa moja kwa moja kwenye Facebook -ulidaiwa kuonyesha athari za kupigwa risasi na polisi kwa Philando Castile katika gari lake Minnesota.
Matukio haya yamezua mjadala mkubwa juu ya ukatili wa polisi nchini Marekani.
Licha ya Jay Z wanamuziki wengine wa Marekani kama Chris Brown, Solange Knowles na Swizz Beatz pia wametoa nyimbo kuhusu mauaji ya kibaguzi nchini Marekani.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!