Friday, 1 April 2016

KONDAKTA ASHITAKIWA KUTISHIA KUMUUA RAIS MAGUFULI


MagufuliImage copyrightStatehouse Tanzania
Image captionMshtakiwa alikuwa kwenye baa ya Soweto eneo la Makumbusho
Kondakta wa daladala amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na shtaka la kutishia kumuua Rais John Magufuli.


Hamim Seif (42) mkazi wa Mwananyamala Ujiji, alidaiwa kutenda kosa hilo Machi 10 mwaka huu katika baa ya Soweto, maeneo ya Makumbusho jijini Dar es Salaam.
Wakili wa serikali Keneth Sekwao aliambia mahakama Alhamisi kuwa mshtakiwa, akiwa katika baa hiyo, alitishia kumuua Dkt Magufuli kwa maneno kwa njia ya kujitoa mhanga.
“Kwa haya mambo anayoyafanya Rais Magufuli, mimi nimo tayari kujilipua kwa kujitoa mhanga ili kumuangamiza,” alinukuliwa na Wakili Sekwao.
Mshtakiwa alikana shtaka hilo.
Hakimu Mkazi, Hellen Liwa aliweka wazi dhamana ya mshtakiwa huyo na kumtaka kutafuta wadhamini wawili, kutoka taasisi ya Serikali inayotambulika, ambao watasaini hati ya dhamana ya Sh2 milioni.
Alishindwa kutimiza masharti ya dhamana na akawekwa rumande hadi 14 Aprili kesi ikatapotajwa tena.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!