Friday, 1 April 2016

EWURA yashusha bei za umeme kwa watumiaji wa viwango tofauti.

Mamlaka ya Usimamizi wa Huduma  za Nishati na Maji EWURA imetangaza kushusha bei za umeme kuanzia leo kwa watumiaji wote wa viwango tofauti.



Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Felix Ngalamgosi wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema wateja majumbani ambao wanamatumizi madogo ya wastani wa uniti  75 kwa mwezi,matumizi yatakayozidi uniti 75 yatatozwa bei ya shilingi 350 kwa kila uniti kwa kila uniti moja inayozidi.
 
Amesema kwa wateja wenye matumizi ya kawaida hususani wateja wa majumbani wenye biashara ndogondogo ikiwemo viwanda vidogo,taa za barabarani,mabango n.k. umeme utatolewa katika msongo mdogo wa umeme kwenye njia moja (230v) na njia tatu (400v) ambapo kwa wateja wenye matumizi ya kawaida ya umeme kupitia  (400v) na matumizi kwa mwezi ni zaidi ya uniti 7,500.
 
Aidha Kushuka kwa bei ya umeme ni kutokana na ombi la Shirika la Umeme Tanzania TANESCO kutaka bei za umeme zipunguzwe sambamba na hilo gharama za huduma kwa baadhi ta wateja zimeondolewa.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!