Vifo vya gafla kwa watoto wachanga imekuwa ni ngumu kwa wazazi kujua nini ni chanzo chake.Kwenye jamii zetu za kiafrika watu wengi huusisha vifo vya watoto na mambo ya ushirikina pale mtoto anapofariki bila kuumwa haswa akiwa usingizini ,sababu wengi hawana elimu ya kutosha juu ya vifo vya gafla. Takwimu inaonyesha watoto wakiume ndio wanaadhiriwa sana kuliko watoto wa kike.Kifo cha gafla kiitalamu huitwa Suddenly Infant Death syndrome ( SIDS) au (Crib death) kinatokea kwa watoto wenye umri 0 mpaka mwaka 1 hutokea pindi wakiwa wamelala .Vifo vingi huwapata sana watoto wenye umri wa 0 mpaka miezi sita na kiasi kidogo kwa wamiezi 6-12.Chanzo chake haijajulikana moja kwa moja ila kunavitu vinavyochochoea kwa kiasi kikubwa,:Kulamza kwa tumbo- ni hatari sababu upumuaji wake unakuwa watabu.:Sigara -uvutaji wa sigara ndani ya nyumba au eneo alilopo mtoto ni hatari mapafu yake hayaja komaa kupokea moshi mkali wenye sumu(NICOTINE) na kumuadhiri kwa haraka.:Watoto wanaozaliwa chini ya wiki 38( njiti) wapo kwenye hatari ya kupata vifo cha gafla:Mama kama alitumia sigara,pombe au bangi kipindi cha ujauzito anauwezo mkubwa wa kumsababishia mtoto kifo cha gafla:Watoto wenye infection kwenye mfumo wa hewa.NJIA ZA KUEPUKA KIFO CHA GAFLA:Mlaze mtoto kwa mgongo-usimlaze ubavu au tumbo sababu position ya kumlazia tumbo inamfanya apate hewa ya oxygen kwa kiasi kidogo inasababisha hewa ishindwe kusafirishwa kwenye ubongo ndio hapo inakuwa rahisi kufariki kwa mtoto. |
Mama anaenyonyesha mtoto kwa kipindi cha mwaka na kuendelea anapunguza hatari ya kifo cha gafla kwa mtoto kwa asilimia 50,kuliko mtoto anaepewa maziwa ya kopo.
:Epuka matumizi ya sigara ndani ya nyumba au sehemu aliopo mtoto
:Mnunulie Pacifier zile chuchu za kunyonya mdomoni zinazuia kifo cha gafla.
Utakapo mlaza kitanda cha watu wazima hakikisha asijigonge ukutani au kusiwe na mpenyo kati ya kindani na ukuta anaweza ingia kati na kukosa hewa na kubanwa.
:Hakikisha kitandani hakuna nguo ,mashuka ,toys,au mto vikamziba pua akakosa hewa wakati wa kujigeuza,na kumbuka mtoto mchanga hana uwezo wa kujitoa shuka iwapo litamfunika uso
:Mtoto kulala kitandani kwake anakuwa safe ,kumwepusha kujigonga kwenye ukuta au angle za kitanda na kuanguka,
:Epuka kumfunika na shuka kubwa au zito ,mtoto anahitaji shuka jepesi ,na iwapo utalala nae hakikisha humfuniki na nguo zako ,au shuka puani akakosa hewa au mwili ukachemka sana.
Nimuhimu kumwangalia mtoto mara kwa mara pindi akiwa amelala,
unaweza ukamnunulia baby monitor inasaidia kumsikia akiwa anapumua,analia ,anacheka n.k inakuwa rahisi kujua kama kuna lolote lineal endelea chumbani.SHUKRANI KWA AFYA YA MAMA NA MTOTO.
No comments:
Post a Comment