Thursday, 4 February 2016

UPEPO MKALI KUIKUMBA TANGA, MAFIA, DAR LEO

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imewataka wananchi wa Ukanda wa Pwani kuchukua tahadhari ya upepo mkali na mawimbi makubwa ya Bahari ya Hindi kuanzia leo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TMA jana jijini Dar es Salaam, ilieleza kuwapo upepo mkali unaozidi kasi ya kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayozidi mita 2.0 kuanzia leo.
Ilitaja maeneo yatakayokubwa na dhahama hiyo ni mwambao wa mikoa ya Tanga, Pwani (ikijumuisha Mafia), Dar es Salaam, Lindi na Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.
Mara kwa mara TMA imekuwa ikitoa tahadhari ya kuwapo kwa mvua, upepo na mawimbi yasiyo ya kawaida na kuwataka wananchi wa maeneo husika hasa wa mabondeni kuchukua tahadhari ikiwamo kuhama maeneo hatarishi.
Januari mwaka huu, TMA ilitoa tahadhari ya uwapo wa mvua nyingi ya kiwango cha Tsunami na kuwataka wananchi wa mabondeni kuyahama makazi yao.
Ilieleza mvua hizo zitaendelea hadi Machi mwaka huu, huku kukiwa na uwezekano mkubwa wa kutokeo tsunami.
Katika mvua zinazoendelea kunyesha nchini, baadhi ya mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Kagera, Geita na Tanga ilikumbwa na mafuriko yaliyosababisha baadhi ya wananchi kupoteza maisha, kujeruhiwa pamoja na mali kupotea.
Mapema Januari mwaka huu, serikali iliendesha ubomoji wa nyumba zilizojengwa kwenye mto Msimbazi jijini, ikiwa ni wananchi wanaishi bondeni na waliotakiwa kuhama.
Jumla ya nyumba 600 ziliwekwa alama ya X na 19,000  zilibomolewa na serikali. Kwa sasa ubomoaji umesitishwa kutokana na kesi iliyofunguliwa na wakazi zaidi ya 600 wa maeneo ya mabondeni kupinga ubomoaji huo.

NIPASHE

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!