Thursday, 4 February 2016

FOS YATOA RIPOTI YA UTAFITI WA USHIRIKISHWAJI WA WANAWAKE KATIKA UCHAGUZI MKUU 2015 JIJINI DAR

Meneja wa Mradi wa kitengo cha haki Jinsia kutoka Oxfam Bi. Rishida shariff akielezea kwa kina namna walivyofanya mradi wa Fahamu Ongea Sikilizwa


 Mtafiti mkuu wa kuhusiana na ushiriki wa wanawake katika uchaguzi mkuu mwaka 2015 Profesa Ruth Meena akifafanua kwa kina namna ya utafiti ulivyofanyika.
 Dkt. Alexander Makulilo kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam akifanya uchambuzi wa namna utafiti ulivyofanyika.
 Aliyekuwa Mgombea wa Kiti cha Urais katika Uchaguzi Mkuu Mwaka 2015 Mama Anna Mgwila akichangia jambo wakati wa uzinduzi huo
 Baadhi ya wawakilishi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi  Zanzibar Idara ya Uratibu Shuguli za SMZ Dar es salaam wa kwanza na wa pili (Kushoto) na Bi. Msangu Said (wa tatu kushoto) kutoka shirika la utangazaji la Zanzibar ZBC
 Baadhi ya wadau waliohudhulia katika uzinduzi wa Ripoti ya ushiriki wa wanawake katika uchaguzi mkuu 2015
 Baadhi ya vijarida na Ripoti
(Picha na Fredy Njeje Blogs za Mikoa)


Kitengo cha Haki za jinsia cha Oxfam nchini Tanzania Fahamu Ongea Sikilizwa(FOS) imezindua kitabu chake cha utafiti kughusu taarifa za kushiriki kwa wanawake kati masuala ya uchaguzi mkuu maka 2015 na 2016 nchini Tanzania.

Uzinduzi wa taarifa hiyo umefanyika jana jijini Dar es salaam katika ukumbi wa Double view na Meneja wa kitengo cha haki za binadamu na jinsia kutoka Oxfam Bi. Rashida Shariff huku akieleza baadhi ya mikoa iliyofanyiwa utafiti huo kuwaTanzania bara kwa mikoa nane ikiwemo Shinyanga, Dodoma, Tanga, Arusha,  Dar es salaam, Morogoro,Lindi na Mwanza na Tanzania visiwani Zanzibar ni Kusini Unguja
Bi. Rashida amebainisha lengo kuu la utafiti huo likiwa ni kuwapauwezo wa kujiamini wanawake kushiriki kikamilifu katika kujitokez kikamilifu kupiga kura pamoja na kujikita kwenye masuala ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi nchini bila woga.

Aidha ameongeza kuwa utafiti umelenga kupata changamoto za wanawake walizokuwa wanapata hususani kwa wagombea ambapo wagombea sita wanawake kutoka katika vyamba mbalimbali vya siasa Mh. Angelina Mabula, Anna Mghwira, Nancy Mrikaria, Khadija Msawira, Magreth Mshenene na Mh. Safia Mkamama wametumiwa kuelezea changamoto zilizowakabili na mafanikio waliyoyapata ikiwemo ni pamoja na kuongeza kujiamini
Kwa upande wake aliyekuwa mgombea urais kwa kupitia Chama cha ACT -Wazalendo Anna Ngwila amesema kuwa ushiriki wa wanawake katika uchaguzi bado umeelekezwa kwenye ushabiki ambapo wanawake hutumiwa katika vyama kwa lengo la kutoa kura zao kuliko wao wenyewe kugombea.
  
Bi Anna akitolea mfano yeye mwenyewe alisema kuwa changamoto aliyokumbana nayo ni ndani ya vyama ilikuwa ni kutiliwa mashaka kama ataweza mikikimikiki ya uchaguzi lakini wanasahau kuwa wanawake nao wanaweza kutatua kero mbalimbali zinazowakabili kijamii.


Naye mtafiti mkuu wa utafiti huo Profesa Luth Meena ameongezea kuwa taarifa hii itasaidia vyombo mbalimbali vya serikali ikiwemo vyama vya siasa, msajili wa vyama vya siasa, tume za uchaguzi, vyombo vya habari, TAKUKURU, pamioja na Asasi za kiraia na jamii kwa ujumla kuzumgumzia kwa usahihi ikiwemo kuchukua hatua za kisera, kisheria katika kuleta usawa wa kijinsia katika michakato ya uchaguzi huku ikiwapa uwezo wa kujiamini kwa wanawake katika kushiriki katika masuala ya uchaguzi.




No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!