Saturday 5 December 2015
KUELEKEA 9/12 SHUGHULI ZA USAFI ZIMEANZA KWA KASI KILA KONA
Hapa ni katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga ambako leo kumefanyika uzinduzi wa wiki ya usafi katika mkoa wa Shinyanga kuelekea siku ya Uhuru Desemba 09,2015 ambayo itakuwa siku kwa ajili ya kufanya usafi nchi nzima ikiwa ni agizo la rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.Leo Jumamosi wafanya kazi wa serikali mkoa wa Shinyanga wakiongozwa na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga wamezindua wiki ya usafi kwa kufanya usafi katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga-Mwadishi wetu Marco Maduhu alikuwepo wakati wa uzinduzi huo..ametuletea Picha 20 kilichojiri...Tazama hapa chini
Viongozi wa mkoa wa Shinyanga wakiongozwa na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga wakijiandaa kuanza kufanya usafi katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga
Kulia ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro (kushoto) wakiongoza zoezi la kufanya usafi kwa kufyeka nyasi katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga
Wa pili kushoto ni mganga wa meno katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga Dkt Daniel Maguja akifuatiwa na mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt Ntuli Kapologwe wakifyeka majani/nyasi
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro,mganga wa meno katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga Dkt Daniel Maguja ,mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt Ntuli Kapologwe na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga wakifyeka nyasi
Tunafanya usafi..lazima tuoneshe mfano kuhimiza wananchi kujua umuhimu wa kufanya usafi.....
Kulia ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akifyeka nyasi ili kuiweka hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga ili iwe safi
Wafanyakazi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga wakifanya usafi
Wafanyakazi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga wakifanya usafi
Wafanyakazi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga wakifanya usafi
Tunafanya usafi kuumunga mkono rais John Magufuli..Hapa Kazi tu!!
Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt Ntuli Kapologwe akifyeka nyasi,kulia ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro....
Kuli ni kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha aliyekuwa ameambatana na askari kadhaa wa jeshi hilo, akiteta jambo na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga wakati wa uzinduzi wa usafi katika mkoa wa Shinyanga
Askari wa jeshi la polisi,wafanyakazi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga na viongozi mbalimbali wa mkoa wakifanya usafi
Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt Ntuli Kapologwe akiushukuru uongozi wa mkoa wa Shinyanga kwa kuanzia kufanya usafi hospitalini hapo ikiwa eneo hilo lilikuwa sio safi hususani kwenye upande wa maeneo ya Ghuba la uchafu, Bima na baadhi ya wodi na sasa maeneo hayo yako safi
Tunabadilishana mawazo baada ya kufanya usafi....
Baada ya usafi...wakijadiliana namna ya kuendeleza zoezi la kufanya usafi mkoani humo,ambapo mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga(mwenye miwani),amesema zoezi hilo litakuwa endelevu, ambapo kila Mwezi usafi utafanyika tarehe 15 na 30 kuanzia saa 12 hadi saa 12 na nusu asubuhi.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga akitafakari jambo baada ya kufanya usafi
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akinena jambo mara baada ya usafi kumalizika katika Hospitali hiyo ya Rufaa, huku akitumia fursa hiyo kuwataka wananchi waige mfano wa viongozi wao na wenyewe wajitokeze kwa wingi kufanya Usafi ili kuhakikisha agizo la rais John Magufuli linatekelezeka kwa asilimia 100
Picha zote na Marco Maduhu-Malunde1 blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment