Ni ugonjwa unaosababishwa na virusi viitwavyo flavivirus. Ugonjwa huu huenezwa na mbu aina ya aedes aegypti na ni vigumu kuutofautisha na magonjwa mengine kama malaria kwenye dalili za mwanzo bila kutumia vipimo. Ugonjwa huu hushambulia seli za kinga mwilini (macrophages, monocytes).
Baada ya kuingia ndani ya seli, virusi vya homa ya manjano huzaliana na kuendelea kukua huku wakihama kutoka kwenye seli moja hadi nyingine kushambulia. Virusi huenda kwenye seli za ini na kuanza kuzishambulia na hivyo kusababisha sumu kwenye damu
Ugonjwa wa homa ya manjano huenezwa na mbu aina ya aedes, ambaye hupatikana katika maeneo ya katika nchi zilizo kusini mwa jangwa la sahara, ikiwemo Tanzania. Mbu jike aina ya aedes hupendelea kunyonya damu pindi awapo mjamzito ili kumwezesha kurutubisha mayai yake. Mbu aliyenyonya damu ya mtu mwenye homa ya manjano huweza kumwambukiza mtu mwingine.
kitropik na savanna, ikiwemo Afrika, amerika ya kusini pamoja na mashariki ya mbali. Mbu hawa kwa Afrika hupatikana zaidi
Ugonjwa huu pia huweza kuenezwa kwa kuchangia sindano na mtu ambaye tayari ameambukizwa ugonjwa wa homa ya manjano na pia kuwekewa damu au kupandikizwa kiungo cha mtu aliyeathirika kunaweza kusababisha maambukizi.
kitropik na savanna, ikiwemo Afrika, amerika ya kusini pamoja na mashariki ya mbali. Mbu hawa kwa Afrika hupatikana zaidi
Ugonjwa huu pia huweza kuenezwa kwa kuchangia sindano na mtu ambaye tayari ameambukizwa ugonjwa wa homa ya manjano na pia kuwekewa damu au kupandikizwa kiungo cha mtu aliyeathirika kunaweza kusababisha maambukizi.
Dalili za homa ya manjano
Mara baada ya kuambukizwa kirusi huyu, kirusi hukaa mwilini na kujizalisha pasipo kuonesha dalili kwa muda wa siku 3 hadi 6 na baad aya hapo dalili zinaweza kuonekana. Dalili zimewekwa katika makundi mawili ambayo ni dalili za awali(za papo) ambazo ni homa, maumivu ya misuli na mgongo, maumivu ya kichwa, kutetemeka , kukosa hamu ya kula, kichefuchefu na kutapika. Wagonjwa wengi hupata uhauheni na dalili hupotea ndani ya siku tatu hadi 4 baada ya dalili kuanza
Hata hivyo asilimia 15 ya watu huingia katika kipindi cha pili ndani ya masaa 24 baada ya dalili za awali kuisha ambapo huonyesha dalili za kipindi cha pili yaani, kujirudia kwa homa kali na kuharibiwa kwa mifumo tofauti ya mwili. Mgonjwa ghafla hupata manjano na hulalamika maumivu ya tumbo na kutapika damu huweza kutoka kwenye mdomo, pua, macho na tumbo. Linapotokea hili damu huonekana kwenye matapishi na kinyesi . kazi za figo hupungua na nusu ya watu walioingia katika kipindi cha dalili hizi hupoteza uhai(HUFA) ndani ya siku 10 hadi 14 na wengine yani nusu huona lakini huwa wameharibiwa ogani mbalimbali mwilini
Homa ya manjano ni ngumu kugundua hasa katika kipindi cha dalili za awali kwa sababu hufanana na magonjwa mengine kama malaria kali, homa ya dengua, virusi vya homa ya ini, na virusi vungine vnavyosababisha kuvuja kwa damu na magonjwa mengine au sumu.kipimo cha damu kinaweza kutambua kinga ya mwili iliyoamaka dhidi ya kirusi cha homa ya manjano. Baadhi ya vipimo hufanywa kwa watu waliokwisha kufa kwa kuchukua maini na ogani zingine ilikutambua virusi hawa lakini huitaji wataalamu waliofundishwa kuhusu mambio ya maabara
Watu walio hatarini ni wapi?
Nchi 44 zenye virusi hawa kwa wastani afrika na latini amerika kwenye watu zaidi ya milioni 900 wapo hatarini kwenye ugonjwa wa virusi hivi. Kwa afrika inakadiliwa watu milioni 508 wanaishi katika nchi 31 zenye virusi hawa. Na nchi zilizobaki yaani 13 zipo huko latini amerika ambapo Bolivia,brazili,coumbia,Ecuador na peru zipo kwenye hatari kubwa
Usafilishaji wa kirusi hawa
Kirusi cha homa ya manjano ni ni aina ya arbovirus ambaye yupo katika genus ya flavivirus. Mbu ni mdudu wa kwanza anayesafilisha ugonjwa huu, hubeba irusi kutoka kwa mtu mmoja kwenda mwingine na awali kati ya nyani na nyani kasha nyani na binadamu na kasha binadamu na binadamu
Matibabu
Hakuna matibabu yaliyo maalumu kwa ajili ya homa ya manjano, matibabu msaada dhidi ya kupoteza maji mengi, kufeli kwa mapafu na homa. Maambukizi nyemelezi ya bakiteria hutibiwa na dawa za zinazopambana na bakiteria. Matibabu msaada huleta matokeo mazuri ingawa hayapatikani katika maeneo masikini
Kuzuia homa ya manjano
Chanjo
Chanjo ni hatua muhimu katika kuhakikisha madhara ya virusi vvya ugonjwa wa homa ya manjano unazuiwa kuwapata watu
Chanjo pia inaweza kutolewa kwa watoto wadogo kama sehemu ya mpango ya kuchanja watoto au katika kampeni za kuwafikia watoto wengi kama vile kuwachanja watoto ndani ya vijiji vyao
Watu gani hawatakiwi kuchanjwa?
Wanawake wajawazito-isipokuwa kama kuna mlipuko wa ugonjwa huu na uwezekana wa mama kuambukizwa ni mkubwa
Watu wenye alegi kwenye protini za mayai
Watu walio na kinga ya mwili ya chini sana kama walioambukizwa VVU na au sababu nyingine au wakiwa na madhaifu katika tezi ya thaimusi
Wasafiri katika nchi haswa za bara asia wanatakiwa kuwa na vyeti vinavyotolewa na shirikalinalijulikana kwamba watu hao wanaoingia bara hila wamekwisha chanjwa dhidi ya virusi vya homa ya manjano
Kudhibiti mbu
Kukata majani yanayozunguka nyumba na kupunguza mazalia ya mbu maeneo kallibu na nyumbani
No comments:
Post a Comment