Thursday, 22 October 2015

JESHI LA POLISI ZANZIBAR WAAHIDI KULINDA USALAMA WA WANANCHI SIKU YA KUPIGA KURA

Jeshi la Polisi Zanzibar pamoja na kuwahidi wananchi kuwa litawalinda na kuhakikisha usalama wao siku ya kupiga kura limewataka wananchi  kuhakikisha wanafuata sheria za nchi kuhusu upigaji na ulinzi wa kura.




Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa jeshi hilo kamisheni ya Zanzibar CP Hamdan Omar Makame wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelezea mikakati ya jeshi hilo kuelekea uchaguzi mkuu jumapili ambapo amesema jeshi litatoa ulinzi wa kutosha kuwalinda wananchi na mali zao lakini ametahadharisha wale ambao wana mpango wa kutaka kubaki maeneo ya upigaji kura kwa madai ya kulinda kura.
Aidha mkuu huyo wa Polisi Zanzibar amesema hakuna kosa lolote linalofanywa na polisi la kushirikaina na vikosi vya SMZ katika kulinda raia na utaratibu huo upo kwa mujibu wa sheria za nchi.
Wakati kumebakia siku nne kabla ya upigaji kura nchini kote jeshi hilo kwa upande wa Zanzibar limekuwamstari wa mbele kuhakikisha wakati wote wa kampeni Zanzibar inakuwa salama ambapo hadi sasa wakazi wa visiwa hivi wameshuudia kamepni zikienda kwa utulivu na bila ya hofu yeyote.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!