Thursday, 6 August 2015

LIPUMBA AJIVUA UENYEKITI CUF




NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

UMOJA wa vyama vinavyounda Katiba ya Wananchi (UKAWA), umeanza kupata pigo baadaya ya Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba kujiuzulu wadhifa huo na kwamba yeye atabaki kuwa mwanachama wa kawaida.


Akizungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya Peacok, jijini Dar es Salaam, Profesa Lipumba alisema ameamua kuchukua umamuzi huo kutokana na Ukawa kushindwa kusimamia makubaliano yao.

Alisema Agosti Mosi mwaka huu kuwa aliiarifu Kamati ya utendaji ya Taifa inayoongozwa na Katibu Mkuu wa chama hicho kuwa atawajibika na kujizulu uenyekiti wa Taifa baada ya wenzake kukamilisha taratibu za ushirikiano ndani ya UKAWA.

Alisema Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Juma Duni Haji, ambaye Baraza Kuu lilimpitisha kuwa mgombea wa uwakilishi jimbo la Bububu amehama chama na kujiunga Chadema na kuteuliwa kuwa mgombea mwenza wa Chadema katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 2015.

“Leo hii nimeikabidhi Ofisi ya Katibu Mkuu barua yangu ya kung’atuka nafasi ya Mwenyekiti wa Taifa lakini naendelea kuwa mwanachama wa CUF na kadi yangu imelipiwa hadi  mwaka 2020,” alisema.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!