Thursday, 6 August 2015
MICHEZO: WACHEZAJI 29 WAITWA TAIFA STARS
KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa leo ametangaza kikosi cha wachezaji 29 watakaongia kambini Agosti 9 mwaka huu katika hoteli ya Tansoma iliyopo Gerezani, Dar es Salaam kwa ajili ya kambi ya wiki moja ya mazoezi.
Kikosi hicho kimewajumuisha wachezaji watano wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi, ambao baadae watajumuika kwa kambi ya kujiandaa kucheza na Nigeria Septemba mwaka huu nchini Uturuki. Taifa Stars inatarajiwa kuweka kambi ya siku kumi Istambul - Uturuki, ambapo itacheza michezo miwili ya kirafiki na timu za Taifa za Libya na Kuwait kabla ya kurejea nchini kuwavaa Nigeria. Wachezaji waliotangazwa na wataingia kambini Jumapili ni makipa, Ally Mustafa ‘Barthez’ wa Yanga SC na Aishi Manula wa Azam FC. Mabeki ni Shomari Kapombe (Azam FC), Michael Aidan (Ruvu Shooting), Juma Abdul, Mwinyi Haji (Yanga SC), Hassan Isihaka (Simba SC), Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Kelvin Yondani (Yanga SC). Viungo ni Himid Mao, Frank Domayo, Mudathir Yahya (Azam FC), Salum Telela (Yanga SC), Abdi Banda na Said Ndemla wote wa Simba SC. Mawinga ni Orgenes Mollel (Aspire – Senegal), Abdrahman Mbambi (Mafunzo), Deus Kaseke, Simon Msuva (Yanga SC), Ramdhani Singano na Farid Mussa (Azam FC), wakati washambuliaji ni John Bocco, Ame Ally (Azam FC) na Rashid Mandawa (Mwadui FC). Wachezaji wanaocheza nje waliojumuishwa katika kikosi hicho ambacho Agosti 23 kitaelekea kambini nchini Uturuki kwa kambi ya siku kumi ni Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu (TP Mazembe – DRC), Mrisho Ngassa (Free State - Afrika Kusini), Hassan Sembi (Santos FC – Afrika Kusini) na Adi Yussuf (Mansfield Town – England).
NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment