MAELFU ya wananchi nchini Uganda jana waliungana na familia, ndugu, jamaa na marafiki kumzika mwanamuziki wa dancehall nchini humo, Emmanuel Mayanja maarufu kwa jina la AK47.
AK47 alifariki dunia usiku wa kuamkia Machi 17, 2015 baada ya kuanguka akiwa bafuni katika baa iitwayo Dejavu, iliyopo eneo la Kabalagala, Uganda.
Maziko ya AK47 yalifanyika katika eneo la Busato, Wilaya ya Mityana nchini Uganda.
(PICHA ZOTE KWA HISANI YA NEWVISION)
No comments:
Post a Comment