Thursday 19 March 2015

KONGAMANO LA MAUAJI YA ALBINO

Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Al-Shaymaa Kwegyir,
akizungumza na wanazuoni wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu cha Hubert Kairuki hawapo pichanai, katika
kongamano la kujadili nini kifanyike kutokomeza mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) lililofanyika jana chuoni hapo. Kushoto ni Makamu
Mkuu wa Chuo hicho Keto Mshigeni na Kulia ni Kokushubika Kairuki.



Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MBUNGE wa Viti Maalum ambaye pia ni mlemavu wa ngozi (albino),
Al -Shaimaa Kweigyir, amekemea vikali
unyanyapaa unaofanywa na baadhi ya Watanzania juu ya jamii yenye ulemavu wa
ngozi na kusema kwamba inawafanya watu hao waishi kwa unyonge.
Mbunge huyo aliyasema hayo jana katika kongamano la kujadili
nini kifanyike ili kutokomeza mauaji na vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa
walemavu wa ngozi llilofanyika katika Chuo Kikuu cha Kumbukumbu cha Hubert
Kairuki na kuhudhuriwa na watu mbalimbali, wakiwamo wanazuoni.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Al-Shaymaa Kwegyir,
katikati akiwa kwenye kongamano la wanazuoni wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu cha Hubert Kairuki kujadili nini kifanyike kutokomeza mauaji ya albino. Kushoto ni Makamu
Mkuu wa Chuo hicho Keto Mshigeni na Kulia ni Kokushubika Kairuki.
Akizungumzia unyanyapaa huo, Shaimar alisema kwamba bado
baadhi ya wana jamii wamekuwa wakiendeleza vitendo vya unyanyapaa vinavyofanywa
na watu ambao wamekuwa na mtizamo hasi juu ya watu wenye ulemavu wa ngozi.
Alisema kwamba jamii ikielimika na kutambua haki sawa kama
walivyokuwa nazo wao juu ya ndugu zao albino, hata mauaji yatapungua kama sio
kwisha kabisa, hususan kwa kuhakikisha kwamba wanawalinda na kuwathamini wakati
wote.
Mbunge wa Viti Maalum CCM, AL Shaimaa Kweigyir kushoto akizungumza na Kokushubika Kairuki katika kongamano hilo lililohudhuriwa na watu mbalimbali.
Baadhi ya wahudhuriaji wa kongamano hilo wakisikiliza mada zilizokuwa zinazungumzwa.
Watu wanasikiliza kwa makini katika kongamano hilo la kujadili juu ya mauaji ya albino yanayoendelea kutokea hapa nchini.
“Wapo watoto wanaozaliwa katika hali ya albino ambao
wamekuwa wakiishi kwa mashaka makubwa kutokana na unyanyapaa dhidi ya jamii
nyingine ambayo ukiangalia kwa kina hakuna tofauti yoyote kati ya albino na
wengineo.
“Naomba jamii ione albino ni watu kama wao kwa kuhakikisha
kwamba wanawathamini, wanawajali na kuwalinda wakati wote, huku wakianzia
kwenye uondoaji wa fikra mgando na unyanyapaa wanaofanya kwa baadhi ya kaya,”
alisema.
Mbunge Shaimar ni
miongoni mwa viongoz wa serikali waliojiweka busy katika kutafuta mbinu za
kuweza kutokomeza mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi albino yanayoendelea
kutokea katika mikoa mbalimbali ya Tanzania.

VIA-FULLSHANGWE BLOG

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!