Wednesday, 28 January 2015

WAZIRI MPYA WA UCHUKUZI SAMUEL SITTA AKUTANA ANA KWA ANA NA WADADA WALIOKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA




Akiwa kwenye ziara ya kutembelea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Waziri mpya wa uchukuzi Samuel Sitta jana alikutana ana kwa ana na wadada waliokamatwa baada ya kukutwa na madawa ya kulevya aina ya heroin waliyomeza tayari kuyasafirisha kwenda HongKong kwa ndege ya Emirates. 

Wadada hao wawili Rehema Ndunguru (32) mkazi wa Sinza mpaka wakati huo alikwishatoa pipi 78 wakati mtuhumiwa mwenzake Moyo Ramadhani alikwishatoa pipi 86 ambapo kazi ya kuwachunguza ilikuwa ikiendelea.

Wanawake hao walidai kuwa kama wangefikisha mzigo huo sehemu husika, kila mmoja angelipwa dola 6.500 (sawa na Sh 11,700,000), ambapo wangepokelewa na tajiri wao ambaye hawajui jina lake, ila angewapigia simu.


No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!