Tuesday, 16 September 2014

TRAFIK AGONGWA AKIONGOZA MAGARI

Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kituo cha Mbagala wilayani Temeke, Koplo Riziki Mohamedi amelazwa katika Hospitali ya Rufani ya Muhimbili baada ya kugongwa na gari akiwa kazini.

Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo aliyekataa kutajwa jina alidai kuwa trafiki huyo alisimamisha gari ghafla na gari la nyuma lililokuwa nyuma likapita bila kusimama na kumgonga na kisha kuyagonga magari mengine yaliyokuwa mbele.
Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Kienya Kienya alisema jana kuwa ajali hiyo ilitokea asubuhi eneo la Mbagala Rangitatu.
Alisema gari aina ya Toyota Hiace inayofanya safari zake kati ya Temeke na Kongowe lilishindwa kufunga breki na kumgonga askari huyo na kisha kuyagonga magari mengine manne yaliyokuwa mbele yake.
Kamanda Kienya alisema katika ajali hiyo, watu wengine sita walijeruhiwa. “Wao walitibiwa na kuruhusiwa kwenda nyumbani. Aliyeumia zaidi ni huyu askari,” alisema Kamanda Kienya.
Alisema Polisi wanaendelea kumsaka dereva wa gari lililosababisha ajali hiyo ili aweze kufikishwa katika vyombo vya sheria, kwani alikimbia baada ya ajali kutokea.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!