Saturday, 5 July 2014

Yanga yaendelea kujifua mchangani chini ya Kocha Marcio Maximo

 Wachezaji wa Timu ya Yanga wakiendelea kujifua kwa nguvu zote kwenye Ufukwe wa Bichi ya Barabara ya Ocean Rodi jijini Dar es Salaam mapema leo asubuhi,ikiwa ni katika maandalizi ya mashindano ya ligi kuu Tanzania Bara inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi hapo Agosti 24 2014.Timu ya Yanga ipo chini ya Kocha aliewahi kuinoa Timu ya Taifa "Taifa Stars" miaka ya nyuma,Kocha Marcio Maximo (wa pili kulia) akiwa na msaidizi wake Leonado Neiva (wa nne kulia) pamoja na Mchezaji wa zamani wa timu hiyo,Salvatory Edward (kulia).Picha zote na Othman Michuzi.


Kocha Marcio Maximo akimueleza jambo mmoja wa Wasaidizi wake ambaye ni Mchezaji wa zamani wa timu ya Yanga,Salvatory Edward.
Kocha Msaidizi wa Timu ya Yanga,Leonado Neiva akitoa maelekezo kwa wachezaji wa Timu ya Yanga,wakati wa Mazoezi yao yaliyoendelea kufanyika leo kwenye Ufukwe wa Bichi ya Barabara ya Ocean Rodi jijini Dar es Salaam.
Kiungo Mshambuliaji wa Timu ya Yanga kutoka nchini Brazil,Andrey Coutinho akishiriki kwenye mazoezi hayo.Kulia ni Mmoja wa Magolikipa wa timu hiyo,Ally Mustafa.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!