Hivi ndivyo Neymar alivyoumia.
Mchezaji wa timu ya Brazil, Neymar hatoendelea
na michuano ya Kombe la Dunia 2014 baada ya kuvunjika mfupa unaoshikana
na uti wa mgongo wakati wa mechi yao na Colombia usiku wa kuamkia leo.
Neymar akilia kwa uchungu baada ya kuvunjika mfupa.
Staa
huyo mwenye mabao manne mpaka sasa kwenye michuano hiyo, alitolewa
uwanjani dakika tatu kabla ya mechi yao dhidi ya Colombia kumalizika.
Neymar akiwa chini baada ya kuvunjika mfupa.
Katika mechi hiyo, Brazil walishinda mabao 2-1 na kutinga Nusu Fainali ambapo watakutana na Ujerumani Julai 8 mwaka huu.
Neymar akipatiwa huduma ya kwanza.
Kwa mujibu wa taarifa za daktari wa timu ya Brazil, Neymar atakaa nje kwa takribani wiki nne.
Neymar akitolewa nje ya uwanja wakati wa Robo Fainali dhidi ya Colombia.
Wapenzi wa soka nchini Brazil wakiwa nje ya hospitali aliyopelekwa Neymar.
1 comment:
aziz bilal00:39
1
Reply
Mchezo umekwisha saa moja zilizopita leo wangesubiri miaka minne ijayo
Post a Comment