Baadhi
ya wanamichezo waliokuwa nchini China kwa ajili ya maandalizi ya
mashindano ya Jumuiya ya Madola wakiwasili katika Uwanja wa ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere jana jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Maendeleo ya Michezo nchini Bw. Leonard Thadeo akisukuma mzizigo ya
baadhi ya makocha wa China waliombatana na Wanamichezo wa Tanzania
waliokuwa China kwa ajili ya mazoezi ya kujiandaa na mashindano ya
Olympic yanayotarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu mjini Glasgow
Scotland, Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo Bibi.
Juliana Yassoda akimpokea mmoja wa wanamichezo hao mara baada ya
kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es
Salaam.
Mkuu
wa Msafara wa Makocha sita kutoka China Bw. Kangkai akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kuwasili katika
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.Makocha hao wa kutoka
China ndiyo ambao walikuwa wakiwafundisha wachezaji wa michezo ya
Riadha, Ngumi na Mpira wa Mezani (Table Tennis) wanamichezo wa Tanzania
waliokwemda nchini humo kwa ajili ya kujiandaa na mashindano ya Olympic
mjini Glasgow Scotland.
Mkuu
wa msafara wa wanamichezo kutoka Tanzania waliokuwa nchini China kwa
ajili ya maandalizi ya mashindano ya Olympic Bw. Boniphace Kimisha
akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani mara baada ya kuwasili
Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Maendeleo ya Michezo Bw. Leonard Thadeo akizungumza na wanamichezo
waliokuwa nchini china kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya Olympic,
mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere jijini Dar es Salaam.
Pichani
Makocha sita kutoka China waliombatana na timu ya wanamichezo wa
Tanzania waliokuwa wameenda nchini China kwa ajili ya maandalizi ya
mashindano ya Olympic yanayotaraji kuanza mapema mwishoni mwa mwezi huu
mjini Glasgow Scotland.Makocha hao wanafundisha michezo ya Riadha, Ngumi
na Table Tenisi.
Mkurugenzi
wa Maendeleo ya Michezo nchini Bw. Leonard Thadeo (wapili kutoka
kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wachezaji na makocho
kutoka china mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa
wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo nchini Bibi. Juliana Yasoda (mwenye
gauni la kitenge) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wachezaji na
makocho kutoka china mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Frank
Shija,-Kitengo cha Mawasiliano Serikalin – WHVUM).
No comments:
Post a Comment