Pages

Thursday, 10 July 2014

WATUHUMIWA WA UTAPELI WA KIMATAIFA WA ZANZIBAR WAFIKISHWA MAHAKAMANI

Watuhumiwa  wa utapeli wa kimataifa wakiwemo raia wawili wa kigeni na mmoja mtanzania wa kutaka kujipatia  shilingi  bilioni 500 kwa njia za udanganyifu kutoka serikali ya mapinduzi ya Zanzibar wamefikishwa  mahakama ya mkoa ya vuga mjini  Zanzibar.



Wakisomewa mashataka mawili mbeleya mrajis wa mahakamakuu Mhe George Kazi watuhumiwa hao Yaqoub Suleiman Khalifa Al mahruky raia wa Oman,Said Abrahman Gamaldin raia wa Marekani na Shiraz  Haroun Jaffer ambaye ni mtanzania kwa pamoja wamesomewa mashataka    yakuwasilisha  hati za udanganyifu na kughushi hati za ahadi ya deni katika ofisi za wizara ya fedha ya Zanzibar mashataka ambayo wote watatu waliyakana na kuomba  kupewa dhamana.maombi ambayo yalikataliwa.
Hata hivyo kabla ya kukataa  kutoa  dhamna waendeshaamshataka  ya serikali  Wahid Mohamed na Omar Sururu waliombakesi hiyo iahirishwe kwa vile upelelezi haujakamilika na huku wakitaka watuhumiwa hao  wasipewe dhamna kwa vile ni wageni na mtanzania pekee anaweza kuingilia upelelzi madai ambayo yalipingwa na jopo la mawakili watatu wa wanowatetea watuhumiwa hao  Abdulah Juma,Said  Hemed na Suleimna  Salum wa mayugwa advocates, madai ambayo yalikataliwa pamoja na Balozi mdogo wa Oman aliyewepo Zanzibar kukubali kumdhanini mtuhumiwa wa Oman, Mhe George Kazi  alikataa hoja za mawakili na kukubaliana na waendesha mashitaka na kuihailisha mpaka julai 26.
wakiongea na ITV mawakili wanowatetea watuhumiwa hao  Said Hemed amesema sheria haikufuatwa kwa vile makosa hayo  yapewa dhamana na swala la wageni halina nguvu huku Abdullah Juma kwa upande wake amesema watakata rufaa mahakama kuu.
Watuhumiwa hao kabla yakukamatwa  waliwasilisha serikalini hati za ahadi za kudai fedha hizo wakiwa na hati zenye saini za Rais mstaafu Amani Abeid Karume,aliyeku waziri wa nchi  fedha Dr.Mwinyihaji Makame na katibu mkuu wizara ya fedha Omar Sheha ambapo hata hivyo Omar Sheha hakuwa katibu mkuu wa fedha wakati wa utawala wa Dr Amani Karume.

No comments:

Post a Comment