Watuhumiwa wa utapeli wa kimataifa wakiwemo raia wawili wa kigeni na mmoja mtanzania wa kutaka kujipatia shilingi bilioni 500 kwa njia za udanganyifu kutoka serikali ya mapinduzi ya Zanzibar wamefikishwa mahakama ya mkoa ya vuga mjini Zanzibar.
Wakisomewa mashataka mawili mbeleya mrajis wa mahakamakuu Mhe George Kazi watuhumiwa hao Yaqoub Suleiman Khalifa Al mahruky raia wa Oman,Said Abrahman Gamaldin raia wa Marekani na Shiraz Haroun Jaffer ambaye ni mtanzania kwa pamoja wamesomewa mashataka yakuwasilisha hati za udanganyifu na kughushi hati za ahadi ya deni katika ofisi za wizara ya fedha ya Zanzibar mashataka ambayo wote watatu waliyakana na kuomba kupewa dhamana.maombi ambayo yalikataliwa.
Hata hivyo kabla ya kukataa kutoa dhamna waendeshaamshataka ya serikali Wahid Mohamed na Omar Sururu waliombakesi hiyo iahirishwe kwa vile upelelezi haujakamilika na huku wakitaka watuhumiwa hao wasipewe dhamna kwa vile ni wageni na mtanzania pekee anaweza kuingilia upelelzi madai ambayo yalipingwa na jopo la mawakili watatu wa wanowatetea watuhumiwa hao Abdulah Juma,Said Hemed na Suleimna Salum wa mayugwa advocates, madai ambayo yalikataliwa pamoja na Balozi mdogo wa Oman aliyewepo Zanzibar kukubali kumdhanini mtuhumiwa wa Oman, Mhe George Kazi alikataa hoja za mawakili na kukubaliana na waendesha mashitaka na kuihailisha mpaka julai 26.
wakiongea na ITV mawakili wanowatetea watuhumiwa hao Said Hemed amesema sheria haikufuatwa kwa vile makosa hayo yapewa dhamana na swala la wageni halina nguvu huku Abdullah Juma kwa upande wake amesema watakata rufaa mahakama kuu.
Watuhumiwa hao kabla yakukamatwa waliwasilisha serikalini hati za ahadi za kudai fedha hizo wakiwa na hati zenye saini za Rais mstaafu Amani Abeid Karume,aliyeku waziri wa nchi fedha Dr.Mwinyihaji Makame na katibu mkuu wizara ya fedha Omar Sheha ambapo hata hivyo Omar Sheha hakuwa katibu mkuu wa fedha wakati wa utawala wa Dr Amani Karume.
No comments:
Post a Comment