Pages

Thursday, 10 July 2014

ALIYEMG'ATA NA KUMCHOMA NA PASI HAUSIGELI AACHIWA KWA DHAMANA



...akijiziba kwa aibu kabla ya kupanda kizimbani.



Amina Said Maige (mwenye miwani) akisubiria kupandishwa kizimbani.

Amina akiwa chini ya ulinzi akisubiri kupanda kizimbani.



Wanaharakati wakiwa nje ya Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni wakifuatilia kesi hiyo.

Wanaharakati wakisubiri kwa hamu kusomwa kwa kesi ya Amina dhidi ya hausigeli wake, Yusta. 

YULE mwanamke anayejulikana kwa jina la Amina Said Maige ambaye anakesi ya kumng’ata na kumchoma kwa pasi hausigeli wake, Yusta  Kashinda (20), ameachiwa kwa dhamana.
Amina alisomewa mashtaka na Wakili wa Serikali, Mohamed Salum mbele ya Hakimu Mkazi, Yohana Yongolo.
Mahakama imemuachi kwa dhamana baada ya masharti yake ya kuwapata waajiriwa wawili pamoja na kiasi cha shilingi milioni tatu kila mmoja kukamilika.
Amina alikamatwa Juni 4 mwaka huu na kufikishwa Kituo cha Polisi Oysterbay kwa kupatikana na kosa la Kumng’ata, kumchoma kwa pasi na kumpiga mwili mzima, Yusta. 

Kesi yake ipo katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, Dar ambapo mara ya kwanza alisomewa mashtaka Juni 12 na kesi kuhairishwa mpaka Juni 26 pamoja na Julai 10.
Kesi yake itasomwa tena Julai 22 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment