Waziri
Wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Chato Mheshimiwa Dkt.John
MagufuliaAkifurahia na wanachama wapya waliojiunga na Chama cha
Mapinduzi CCM katika kata ya Kasenga katika Jimbo la Chato Mkoani Geita.
Waziri
wa Ujenzi ambaye pia ni mbunge wa Chato Mheshimiwa Dkt.John Pombe
Magufuli akitoa maelekezo kwa Mkuu wa wilaya ya Chato Rodrick Mpogolo
wa pili kutoka kushoto pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya
Chato Ndugu Clement Berege (wakwanza kulia). wa kwanza kushoto ni Ndugu
Ibrahim Bagura Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Chato.
Waziri
Wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Chato Mheshimiwa Dkt.John
Magufuli akizungumza na Mkuu wa wilaya ya Chato Rodrick Mpogolo katika
ziara yake Kata ya Kachwamba.
Na Mwandishi wetu
Mbunge
wa Chato ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe
Magufuli amewaasa Wananchi Jimbo la Chato Mkoani Geita kufanya kazi kwa
bidii na ushirikiano bila kujali itakadi zao za kisiasa.
Dkt.
Magufuli aliyasema hayo jana katika mikutano yake ya kuhamasisha
maendeleo katika kata za Kasenga, Ichwankima na Kachwamba wilayani Chato
katika mkoa wa Geita.
“Ndugu
zangu tufanye kazi kwa bidii, maendeleo hayaji hivi hivi, tuache
malumbano na itikadi zetu za vyama ili tujenge jimbo letu vizuri”
Alisema Waziri Magufuli
Dkt.
Magufuli aliongeza kuwa Serikali ya CCM haina ubaguzi ndio maana
inapeleka maendeleo katika maeneo yote na hata yale yanayongozwa na
wapinzani.
“Mnatakiwa
kushirikiana na Serekali na sio kubeza kama watu wengine wanavyofanya.
Serikali yetu imefanya mambo mengi mazuri ya kuwaletea maendeleo”
alisisitiza Mheshimiwa Waziri
Katika
hatua nyingine Waziri Magufuli alimtaka Mhandisi wa Halmashauri ya
Wilaya ya Chato ndugu Peter Ngunula kuhakikisha kuwa ndani ya miezi
miwili wananchi wa kata ya Kasenga waanze kupata maji kama awali.
“Mhandisi
naomba baada ya miezi miwili wananchi hawa waanze kupata maji kama
awali, na wananchi mtunze miundombinu ya maji haya ili tuweze kutatua
kero hii kwa pamoja” alisema Waziri Magufuli
Katika kusisitiza jambo hilo Waziri Magufuli alichangia shilingi milioni moja ili zisaidie katika tatizo hilo la maji
Katika
hatua nyingine, waziri Magufuli aliwaahidi wakazi hao kuwa Serikali
imeanza mchakato wa kuwaletea umeme na wajiandae na fedha kidogo tu
Shilingi elfu ishirini na saba 27000/= kwa ajili ya uunganishaji.
Serikali
imedhamiria kuwasaidia na kushusha gharama za uunganishaji umeme ndio
maana kipindi kile tunaunganisha umeme pale Chato gharama zilikuwa
shilingi laki nne na nusu.
No comments:
Post a Comment