Rais Jakaya Kikwete amesema serikali imetenga kwa kila halmashauri ya wilaya nchini kupatiwa shilingi milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za walimu ili kuwapunguzia adha na usumbufu walimu wanapopangiwa kwenda katika vituo vya kazi wanakosa mahali pa kuishi.
Rais Kikwete ametoa ahadi hiyo wakati akizungumza na viongozi wa serikali,chama na wananchi wa tarafa ya Kimbe iliyopo wilayani Kilindi wakatia akifungua maabara zinazojengwa chini ya sera ya kutaka kila shule ya sekondari iwe na maabara ili kuwanufaisha wanafunzi waweze kusoma masomo ya sayansi kwa manufaa yao na taifa kwa ujumla.
Kuhusu ujenzi wa shule za kata ambao amedai kuwa awali zoezi hilo lilipuuzwa na kuitwa shule za yebo yebo,rais Kikwete amesema ni shule zinazowaunganisha Watanzania tofauti na awali wanafunzi kufaulu ilikuwa ni kwa baadhi ya shule nandio maana serikali imeanza kujenga shule hizo kisha kusomesha idadi kubwa ya walimu ikifatiwa na maabara ili kuweka uwiano kielimu nchini.
Awali akielezea changamoto wanazokabiliana nazo wakazi wa tarafa ya Kimbe wilayani Kilindi,mbunge wa jimbo hilo mheshimiwa Beatrice Shelukindo amesema wakazi wa eneno hilo wanalazimika kuuza debe moja la mahindi kwa shilingi 2,400/= hivyo amemuomba rais Kikwete kuwashawishi hifadhi ya taifa ya chakula kununua mazao yao ili kunusuru nguvu za wakulima zisipotee bure
This comment has been removed by a blog administrator.
ReplyDeleteaziz bilal14:30
ReplyDelete1
Move nzuri sana imefanywa na serikali yetu