Watu 42 wamejeruhiwa,21 kati yao wakiwa na hali mbaya,baada ya basi la kampuni ya SB lililokuwa linatokea Mtwara kwenda Dar es salaam kupata ajali eneo la Mchinga-Lindi.
WAKATI HUO HUO--
Basi la Amani Express likitokea Kigoma kuelekea Dar es salaam limepata ajali usku wa kuamkia leo maeneo ya Salanda mkoani Tabora, ambapo mtoto wa miaka mitatu amepoteza maisha na abiria kadhaa wamepata majeraha. Mashuhuda wanahisi kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi. Pichani abiria wakitafuta vitu vyao
Baadhi ya abiria walionusurika katika ajali hiyo wakisubiri msaada wa usafiri
Basi la Amani likiwa limepinduka
Kikosi kazi cha Michuzi TV kilicho katika ziara ya kikazi mikoani kikihojiana na baadhi ya abiria asubuhi hii
No comments:
Post a Comment