Sunday, 22 June 2014

MENGI KUFUNDA WANAWAKE WAJASILIMALI



MFUKO wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) unatarajia kutoa mafunzo kwa wanawake wajasiriamali jijini Dar es Salaam ambapo Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi atakuwa miongoni mwa watoa mada.



Mkurugenzi Mtendaji, wa mfuko huo, Stephen Emmanuel alisema mafunzo hayo yatafanyika kwa siku tatu kuanzia keshokutwa katika ukumbi wa JKT Mgulani, Temeke jijini Dar es Salaam.
“Lengo la mafunzo haya kwa mwaka huu ni kuwaelimisha wanawake jinsi ya kupata mitaji kwa ajili ya biashara, masoko pamoja na stadi za ujasiriamali,”alisema.
Katika semina hiyo mada kuu zitahusu Uwekezaji na Ukuzaji mtaji, Utunzaji wa Kumbukumbu za Biashara kwa Kutumia Mashine za Elektroniki(EFDs), Kuwaunganisha Wazalishaji na Masoko, Mbinu za kushiriki Maonesho ya Biashara, Utaalamu wa Kusindika Mazao, Usajili na Matumizi ya “Bar Code” na nyinginezo.
Aidha, elimu juu ya maradhi sugu yanayorudisha nyuma maendeleo ya wanawake itatolewa na jinsi ya kujikinga dhidi ya Malaria, Dengue, Saratani ya Matiti na Shingo ya Uzazi pamoja na Fistula.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!