Sunday, 22 June 2014

EGPAF, VVU BADO NI TATIZO

WAANDISHI wa habari wametakiwa kuandika hali halisi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU) kutoka mama kwenda kwa mtoto kwani bado ni tatizo kubwa nchini.

Hayo yalibainishwa na mwezeshaji kwenye semina ya siku mbili, Charles Kayole, iliyolenga kuwajengea uwezo wanahabari namna ya kuandika na kuripoti habari za EMTCT iliyoandaliwa na shirika lilisilo la kiserikali la EGPAF wilayani Bagamoyo.
Programu ya kutokomeza maambukizi ya VVU toka kwa mama kwenda kwa mtoto (EMTCT) inayosimamiwa na Shirika la EGPAF kwa ufadhili wa   watu wa Marekani kupitia Centre for Diseases Control and Prevention (CDC) na USAID inalenga kutokomeza maambukizi hayo.
Kayole alisema hali ya maambukizi ya VVU toka kwa mama kwenda kwa mtoto bado ni tatizo kubwa nchini, hivyo wanahabari wanapaswa kuujulisha umma hali ilivyo mbaya kwa sasa.
“Ndugu zangu wanahabari hali ya maambukizi ya VVU toka kwa mama kwenda kwa mtoto ni mbaya… tuachane na uandishi wa mazoea, tuujulishe umma mambo yalivyo.
“Siku zote wanahabari wanaona habari nzuri ni kashfa za viongozi, watu maarufu, wanasiasa na uchumi, lakini wanasahau hali mbaya ya watoto na mama zetu,” alisema.
Aliongeza kuwa wanahabari wanapaswa kuandika taarifa mpya, sio kila siku zile zile tu na  kwamba wanapaswa kuongeza uwezo kila mara ili kufikia malengo ya wale wanawaona kama kioo cha jamii.
TZ-DAIMA

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!