MGANGA mmoja wa jadi, hivi karibuni alikusanya umati mkubwa wa watu baada ya kuinyeshwa dawa familia nzima ya mwanamke aliyemleta kwa lengo la kumfanyia uganga ili kumrejesha mtoto wake aliyepotea katika mazingira ya kutatanisha mjini hapa.
Mwajuma Bakari Tindwa mwenye umri wa miaka 52, mkazi wa Mwembesongo aliyemleta mganga akiandaliwa dawa ili kumrejesha mtoto aliyepotea.
Tukio hilo lilitokea Jumamosi ya wiki iliyopita baada ya Mwajuma Bakari Tindwa mwenye umri wa miaka 52, mkazi wa Mwembesongo kumleta mganga huyo, Omar Ally ili amrudishe mtoto Omar Abdul Matenda (10), mwanafunzi wa darasa la nne katika Shule ya Msingi Uhuru, aliyepotea Juni 8, mwaka huu.
Mwajuma aliliambia gazeti hili kuwa mwanaye alipotea katika mazingira ya kutatanisha na kwa zaidi ya wiki tatu, wamekuwa wakimtafuta bila mafanikio.
“Baada ya kumkosa kote huko nilitoa ripoti Kituo cha Polisi Msamvu na kituo kikuu cha polisi nao wamehangaika bila mafanikio, baada ya kujadiliana na familia yangu tuliamua kumchukua huyu mganga ambaye alituhakikishia kumrejesha mwanangu,” alisema.
Alipotakiwa kuzungumzia mazingira ya mtoto huyo kupotea, alisema alikuwa akicheza na mwenzake ambaye pia anaitwa Omar, lakini mwenzake alirudi na kudai rafikiye amepotea kiajabu.
Mganga huyo aliyefika hapo akiwa na timu ya watu wanne, alisababisha umati wa watu kujaa kushuhudia alichokuwa akikifanya, ikiwa ni pamoja na kumchinja paka na kuinywa damu yake, kuchimba shimo mithili ya kaburi nje ya nyumba na kufukia msalaba.
...Timu nzima ya waganga waliofika kutoa huduma kwa Bi. Mwajuma Bakari Tindwa ili kumrejesha mtoto aliyepotea.
Aidha, akitumia kifaa kama darubini, alimulika na kwenda nyuma ya nyumba ambako alichimba na kutoa mapembe mawili, vitu ambavyo hata hivyo, havikuwezesha kurejea kwa mtoto huyo.
“Tulipofika hapa mtoto alikuwa jirani kwa mujibu wa vifaa vyangu, lakini sasa wamempeleka umbali wa mita 250 hivyo kwa sasa tunaingia ndani na kufanya shughuli zetu kwenye nyumba hii na baadaye tutaendelea na kazi ya kumrejesha,” alisema mganga huyo baada ya kuona sura za watu zikiwa kama zinazouliza.
Katika hali ya kushangaza, mganga huyo alikutwa akiwa na picha za marais watatu wastaafu, Baba wa Taifa na Ali Hassan Mwinyi sambamba na ya Rais Jakaya Kikwete. Hadi Uwazi linaondoka eneo la tukio, mtoto Omar hakuwa amepatikana.
CHANZO-GPL
1 comment:
Emmanuel Amose03:28
1
Svara
wajinga ndio waliwao..
Post a Comment