Mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali, Ludovick Utouh akikmabidhi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete Tuzo maalum kwa kutambua mchango wange kwa taasisi simamizi katika kuimarisha Uwazi, Uadilifu na uwajibikaji wakati wa hafla maalum ya chakula cha jioni iliyofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano Julius Nyerere(JNICC) jijini Dar es Salaam jana jioni.
Bwana Utouh alikabidhi Tuzo hiyo kwa niaba ya taasisi sita ambazo ni Bodi ya Taifa ya wahasibu na wakaguzi, TAKUKURU, Mamlaka ya Udhibiti na Ununuzi wa Umma, Mamlaka ya udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya jamii, Mkaguzi wa ndani Mkuu wa Serikali na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa umma.
(Picha na FreddyMaro).
No comments:
Post a Comment