Sunday, 5 January 2014
RAIS KIKWETE NA MAKAMU DKT MOHAMED BILAL WAWAONGOZA WANANCHI KUTOA HESHIMA ZA MWSHO KWA ALIYEKUWA WAZIRI WA FEDHA MAREHEMU DKT WILLIAM MGIMWA KATIKA VIWANJA VYA KARIMJEE DAR
Rais Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakitoa heshima zao za mwisho mbeleya jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Waziri wa Fedha Dkt William Mgimwa, wakati wa shughuli za kuaga mwili zilizofanyika, kwenye viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam leo mchana, mwili wa marehemu umesafirishwa leo kwenda mkoani Iringa kwa mazishi.
Makamu wa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Mohamed Gharib Bilal na mkewe Mama Zhakia Bilal wakitoa heshima zao za mwisho, mbele ya jeneza lenye mwili wa aliyekuwa waziri wa Fedha marehemu Dkt William Mgimwa mapema leo...
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Mohamed Gharib Bilal, na mkewe Mama Zhakia Bilal, wakiifariji familia ya Dkt William Mgimwa.
Rais Kikwete akiifariji familia ya Marehemu Dkt William Mgimwa, mapema leo wakati wa kuaga na kutoa heshima za mwisho, katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Mawaziri mbalimbali wakibeba jeneza na kutoa heshima zao za mwisho, kabla ya mwili wa marehemu kusafirishwa kuelekea mkoani Iringa kwa mazishi.
Mama Maria Nyerere akitoa heshima zake za mwisho
Spika wa Bunge Anne Makinda, akitoa heshima za mwisho.
Katibu mkuu wa CCM, Abdrahman Kinana akitoa heshima za mwsho.
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe, akitoa heshima za mwisho
Baadhi ya Mawaziri wakitoa heshima zao
Viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa ...
Viongozi mbalimbali walishiriki
Mwili ukipakiwa kwenye gari, tayari kwa safari kuelekea mkoani Iringa kwa mazishi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment