Mwanvita Makamba ni mtu ambaye amekuwa mstari wa mbele sana katika swala zima la vita juu ya umasikini, na si Tanzania pekee hata nje ya Tanzania, mchango wake mkubwa umelenga kwa watu wa hali tofauti haswa watoto, ambao wanaishi katika mazingira magumu, huyu dada ametumia muda wake mwingi kutembelea watoto mbalimbali, wengi wao mayatima, na hata wale wa nchi jirani kama Congo, ambao kwa kiasi kikubwa wameathirika sana na vita..bila konyesha dharau amechangia kuwapa moyo, na misaada mbalimbali. kwa mtazamo wangu Mwanvita Makamba ni mfano wa kuigwa.....
A day in Goma, letting her try my pair of sun glasses.
This 2 years old baby was raped, with her mum.
Emotional day in Mugunga Refugees Camp. I believe he'll
still grow up with dreams and make it in life. Touching!
BILA KUSAHAU HAWA AKINA DADA JOYCE KIRIA, NA HOYCE TEMU..
Joyce amefanya Wanawake kutambua thamani yetu, ambayo wengi wetu hatukuijua na zaidi amefanya tutambulike umuhimu wetu katika jamii, na pia amefanya tuweze kujiamini.. yote haya kupitia kipindi chake cha "Wanawake live" ameweza kufichua maovu, manyanyaso wanayotendewa wanawake, ndani ya ndoa na hata nje ya ndoa, wasichana wadogo wengi wameelimika kupitia kipindi chake, amekemea unyanyasaji dhidi ya wanawake na watoto, Kipindi hicho kimeweza kumfanya mwanamke ajithamini, na kuweza kusimama peke yake, yeye kama yeye... Ni mwanamke ambaye anahitaji pongezi kwa kutuwakilisha wanawake....
HOYCE TEMU..
Ameweza kufukua mengi yaliyojificha chini ya uvungu, yaliyokuwa hayajulikani na wengi wetu, kuhusiana na maisha ya watu mbalimbali wasiojiweza kimaisha, kuanzia Afya malazi, na makazi..mijini na vijijini, kipindi chake cha mimi na Tanzania kimeamsha hisia na kuwagusa walio,wengi mmojawapo mimi mwenyewe.. Ameweza kuhamasisha utoaji wa misaada kwa wagonjwa na vilema wasiojiweza, kwa kufanya hivyo amesaidia watu wengi kupata misaada mbalimbali ikiwemo matibabu na mengineyo, wagonjwa wengi, (haswa watoto) wamepata uwezo kutibiwa nje ya nchi kutokana na misaada iliyotolewa kupitia kipindi chake cha Mimi na Tanzania.
Nampongeza sana kwa kuwa alitumia kipaji chake cha kuwa missTanzania kwa kuwasaidia wasiojiweza, na si kwa faida yake Binafsi....
NASEEB ABDUL(DIAMOND...
NI MSANII AMBAYE AMEONYESHA MFANO MZURI KWA JAMII, AMEKUWA MSTARI WA MBELE KATIKA KUSAIDIA WATOTO YATIMA NA WASIOJIWEZA,..AMETUMIA KIPAJI CHAKE KUELIMISHA JAMII,NA KUKUMBUSHA KUWA HATA KIDOGO ULICHONACHO, CHAWEZA KULETA TOFAUTTI KWA YULE AMBAYE HANA KABISA..
Diamond atembelea kituo cha watoto yatima na kula nao kwa pamoja, ikiwa ni kituo kati ya vituo vya mayatima alivyotembelea na kuungana nao wakati wa sherehe za krismas, na pia ametoa misaada mbalimbali katika vituo hivyo..
Diamond Platinumz amerudisha fadhila kwa jamii kwa kuwatembelea watoto yatima waliopo Buguruni jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment