NA MILLARD AYO
Saa tano asubuhi leo zimetoka taarifa za abiria wapatao kumi kurushwa ghafla baharini baada ya boti waliyokua wakisafiria kutoka Pemba kwenda Unguja kupatwa na dhoruba ya upepo mkali kwenye eneo hatari la Nungwi huku maelezo ya abiria waliohojiwa yakisema watu hao ilibidi waachwe ili boti nzima isizame lakini wakatupiwa maboya ya kujiokoa.
millardayo.com imempata msemaji wa Polisi Zanzibar ambae anasema ‘ni kweli kuna boti ya Kilimanjaro II iliondoka Pemba kwenda Znz saa mbili na dakika 20 asubuhi ikiwa na abiria 369 Wakubwa, abiria wadogo 60 na mabaharia Wanane na kwamba boti hii ilipofika kwenye eneo hatari la Nungwi saa nne na dakika 15 ilipata dhoruba kutokana na upepo mkali’
‘Baada ya muda kidogo wakati wa tukio hili kuna baadhi ya abiria walichukua life jacket 5 na kuzitupa baharini bila maelekezo ya nahodha au bila kupata amri kutoka kwa Wafanyakazi wa meli hiyo ambapo baada ya tukio hili boti iliendelea na safari na kufika salama na abiria wake Znz saa tano na dakika 50′
No comments:
Post a Comment