1557571_562004543891688_415853806_n
Wananchi wenye hasira kali Kiwalani wakitoa kipigo cha Mbwa Mwizi kwa Vijana wawili wanaosadikiwa kuwa ni vibaka, wanaosumbua mitaani kwa kuiba na kukwapua, Vibaka hao wanajiita watoto wa Mbwa jumla ya idadi yao ni 40 ambapo mpaka sasa Vibaka 6 wameshauliwa na wananchi wa Kiwalani.

Hadi mdau wa habari hizi anaondoka eneo la tukio aliwaacha vijana hao wameshaaga dunia kufuatia kipindo kikali kilichoambatana na Mawe, matofali, mashoka, Nondo na vifaa vingine vyenye ncha kali.
1526639_562001980558611_1882455163_n
 Vibaka hao wakiwa wanachuruzika damu kutokana na kipigo kikali.

1536683_562002240558585_1659833267_n
Wakazi wa Kiwalini wakubwa kwa wadogo wakiwa wamefurika eneo la tukio. (Picha shukrani kwa Mdau Vasmo Onesmo)

Kwa mtazamo wangu, hivi mtu yeyote akiwa na kisa nawe akakuitia mwizi, na watu wanatoka wakakupiga kama hivi inavyoonekana kwenye picha, nyiemnaopiga mnaushahidi gani? kuna habari nilitoa siku za nyuma kijana aliitiwa mwizi, akapigwa vibaya mpaka kufa, hii inadhihirisha ni kiasi gani tumekuwa na roho za kinyama, jamani kuna polisi kwanini hamuwakamati na kuwapeleleka polisi?  mnaamua kuchukua sheria mkononi,  mnaua mtu kaiba kuku, mkaa?  tubadilike tuwe na roho za kibinadamu