Taarifa zinaarifu kuwa karibu watu 4 huenda wamefriki katika shambulizi hilo na wengine kadhaa kujeruhiwa.
Shirika la msalaba mwekundu limesema kuwa watu 15 waliojeruhiwa walipelekwa hospitalini.
Hata hivyo polisi hawajatangaza idadi rasmi ya watu waliojeruhiwa wala wale waliofariki.
Mlipuko huo umesemekana kutokea ndani ya matatu iliyokuwa inakwenda katika mtaa wa Eastleigh ambao una idadi kubwa ya wasomali wanaoishi huko.
Athari za mlipuko huo hazikuyasaza magari mengine manne yaliyokuwa karibu na matatu hiyo.
Polisi walilazimika kutumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya watu waliokusanyika katika eneo la shambulizi kujionea yaliyokuwa yanajiri.
BBC SWAHILI.
BBC SWAHILI.
No comments:
Post a Comment