Sunday, 15 December 2013
MWENYEKITI WA CCM MKOANI MWANZA AUAWA
CLEMENT MABINA.
Aliyekuwa mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza ndg CLEMENT MABINA ameuwawa na wananchi wenye hasira kali kwa kupigwa mawe huko maeneo ya Kiseke jijini Mwanza.
Chanzo cha kuuwawa ni kwamba mabina aliwanyang'anya ardhi wananchi hao na kesi ikawa mahakamani na leo mchana Mabina bila kibali cha mahakama alikuwa anapanda miti na kujenga msingi wa nyumba ndipo wanachi wakaenda kumhoji iweje anapanda miti na kuweka msingi kwenye viwanja hivyo ilhali kesi ipo mahakamani?
Mabina akaanza kutoa lugha chafu na kurusha risasi hewani...
Risasi zilipomuishia na kufanikiwa kumuua raia mmoja 1 kwa risasi ndipo wananchi wenye hasira kali wakamrudia kumpiga wakiwa na mapanga, mawe na kila silaha ya kijadi, jambo lililopelekea umauti kumkuta. Mauaji yametokea leo mchana majira ya saa 7.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment