Thursday 12 December 2013

TANZANIA IMESEMAJE KUHUSU KUILAZIMISHA UGANDA KUTUMIA BANDARI YA DAR ES SALAAM?



Hii ni wakati Hayati Mwl. Nyerere akiongea na Wanajeshi wa Tanzania wakati wa vita ya Uganda na Tanzania.
Hii ni wakati Hayati Mwl. Nyerere akiongea na Wanajeshi wa Tanzania wakati wa vita ya Uganda na Tanzania.

Kabla ya yote, unapaswa kujua kwamba Tanzania inaidai Uganda dola za Kimarekani milioni nane (8.824) baada ya kulipwa milioni 9.656 kama fidia za athari za vita ya Uganda na Tanzania.
Baada ya headlines za Uganda kuwa kitu kimoja na Rwanda kwenye ishu juu ya utumiaji wa bandari ya Dar es salaam, serikali ya Tanzania imesema haitailazimisha Uganda kutumia bandari hii.
Kwenye bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania December 11 2013, Mbunge wa Mbinga magharibi Capt. John Komba aliuliza swali kwa Waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa Shamsi Vuai Nahodha.
Capt. Komba: ‘Kwa kuwa Serikali ya Uganda inashirikiana na Rwanda kuihama bandari yetu, kwa nini serikali ya Tanzania isiilazimishe Uganda kutumia bandari yetu mpaka deni liishe? Serikali haioni kwamba ni wakati muafaka sasa kumkumbusha Rais Museveni kwamba ilimpa hifadhi ya kisiasa?
Shamsi Vuai Nahodha : ‘Tanzania ni nchi ya pekee na ina bahati sana ya kuwa na viongozi wa aina ya Mwalimu Nyerere, haiingii maanani kwa mtu kumsaidia ndugu yake jana lakini wanavyotofautiana mawazo leo, anamdai yale mambo ambayo aliyafanya nyuma’
NA MILLARD AYO.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!