Thursday 12 December 2013

MANDELA AKUTANISHA MAHASIMU



Katika uhai wake mpambanaji dhidi ya ubaguzi wa rangi duniani, Nelson Mandela, aliishangaza Dunia alipotangaza msamaha kwa waliomtesa na akiwa marehemu, amekutanisha viongozi maadui wa kisiasa duniani katika uwanja mmoja wakimuaga. 

Katika hafla ya jana, Rais Robert Mugabe alijikuta akikutana na mahasimu wake kisiasa, Rais Barack Obama na Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron. Obama na Cameron waliweka vikwazo vya kiuchumi kwa Zimbabwe wakipinga matokeo ya uchaguzi uliompa Mugabe ushindi wa asilimia 61 dhidi ya wapinzani wake, wakidai kuwa kiongozi huyo alichakachua kura.

Aidha, Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Natanyahu ambaye awali aliripotiwa kutokwenda, alifika na kukaa katika uwanja mmoja na Rais wa Mamlaka ya Palestina, Mahmoud Abbas, licha ya kuwa na ugomvi wa muda mrefu na unaoendelea baina yao.

Pia Rais Obama, alikutana na Rais Raul Castrol wa Cuba, ambapo uhusiano baina ya nchi hizo umekuwa ukidorora tangu Mapinduzi ya Cuba ya mwaka 1959. Kutokana na uhusiano mbovu kati ya nchi hizo, mpaka leo Marekani haina uhusiano wa kibalozi na Cuba, huku nchi hiyo ikiweka katika sheria zake vizuizi kwa kampuni za Marekani kufanya biashara na Cuba.

Lakini pia historia iliandikwa katika tukio hili baada ya Marais wane wa Marekani Jimmy Carter, Clinton, Bush na Obama kukutana kwa wakati mmoja katika Ardhi ya Afrika

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!