Kamishna
wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Suleiman Kova akiwaonyesha
waandishi wa habari mapanga waliyoyakamata wakati wa msako mkali wa
kuwasaka watuhumiwa waliomvamia na kumshambulia Dk Sengondo Mvungi
Mjumbe wa Tume ya Katiba. Katika msakao huo watuhumiwa tisa walikamatwa
wakiwa na mapanga na simu moja ya mkononi. Katikati (waliokaa meza kuu)
ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi. Kushoto ni
Naibu Waziri wa wizara hiyo, Pereira Ame Silima. Hata hivyo, Waziri
Nchimbi aliwaomba wananchi na waandishi wa habari wawe na subira wakati
Jeshi la Polisi likiendelea na uchunguzi kwa ajili ya kuwakamata
watuhumiwa wengine. Mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam leo.
Sehemu
ya waandishi habari waliohudhuria mkutano wa Waziri wa Mambo ya Ndani
ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi alipokuwa anazungumza na waandishi wa
vyombo mbalimbali vya habari vya nchini na nje ya nchi kuhusiana na
tukio la kuvamiwa na kushambuliwa Dk Sengondo Mvungi, Mjumbe wa Tume ya
Katiba. Waziri Nchimbi alisema upepelezi wa tukio hilo umefanikiwa kwa
zaidi ya asilimia 80 ambapo tayari watuhumiwa tisa wamekamatwa wakiwa na
mapanga na simu moja ya mkononi, watuhumiwa hao walitajwa majina yao
katika mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi, jijini Dar es Salaam leo. Hata hivyo, Waziri Nchimbi aliwaomba
wananchi na waandishi wa habari wawe na subira wakati Jeshi la Polisi
likiendelea na uchunguzi kwa ajili ya kuwakamata watuhumiwa wengine.
No comments:
Post a Comment