Tuesday, 12 November 2013

MKE WA RAIS MAMA KIKWETE AFUNGUA RASMI WARSHA YA VIONGOZI WA KIMILA KUHUSU AFYA YA UZAZI NA KUZUIA MAAMBUKIZO YA UKIMWI.




Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akifungua rasmi warsha ya siku moja ya viongozi wa kimila wa jamii ya wafugaji kuhusu afya ya uzazi na kuzuia maambukizi ya ukimwi iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere hapa Dar tarehe 9.11.2013.



Mke wa RaiS Mama Salma Kikwete akivishwa mavazi ya wafugaji wa jamii ya wamasai wakati wa warsha ya viongozi wa kimila iliyofanyika Dar tarehe 9.11.2013. Baadaye Mama Salma alipokea zawadi kwa ajili ya Mheshimiwa Rais Dkt. Jakaya Kikwete.
kwa picha zaidi bofya soma zaidi.




Baadhi ya washiriki wa warsha ya viongozi wa kimila wa jamii ya ufugaji kuhusu afya ya uzazi na kuzuia maambukizi ya ukimwi wanaonekana wakisikiliza kwa makini mambo yaliyokuwa yakiongelewa kwenye warsha hiyo.

Baadhi ya wafugaji wa jamii ya wamasai wakicheza ngoma za asili wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar tarehe 9.11.2013.


Olaiboni (CHIFU) wa Kabila la Wamasai Bwana Tikwa 
Moreto akizungumza na washiriki wa warsha.


Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifanya mazungumzo na Oloiboni Bwana Tikwa Moreto wakati wa warsha.

Katibu Mtendaji wa WAMA Bwana Daud Nassib akizungumza na wajumbe wa warsha ya viongozi wa kimila wa jamii ya wafugaji hapa nchini iliyofanyika tarehe 9.11.2013.



Baadhi ya washiriki wa warsha ya viongozi wa kimila wa jamii ya wafugaji wqakisikiliza kwa makini hotuba ya ufunguzi iliyokuwa ikitolewa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere tarehe 9 11.2013.
(PICHA NA JOHN LUKUWI)



No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!