Tuesday, 12 November 2013

MFANYABIASHARA AFARIKI GHAFLA NDANI YA DALADALA AKITOKEA BAGAMOYO KUELEKEA DAR..



MKAZI wa Mapinga wilayani Bagamoyo, Pwani, Daniel Busianya (58), alindondoka na kufariki alipokuwa amekaa kwenye kiti akisafiri kwenda jijini Dar es Salaam.
 
 Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura, alisema tukio hilo lilitokea juzi, saa 3.00 asubuhi maeneo ya Mbuyuni njia panda ya Kunduchi, Kata ya Kilongawima.
 
 Kwa mujibu wa msemaji mkuu bwana Wambura,  Busianya ambaye ni mfanyabiashara alikuwa anatokea nyumbani kwake Mapinga Bagamoyo kwenda jijini Dar es Salaam na alipofika Kunduchi ghafla alianguka kwenye kiti alichokuwa amekaa na kufariki papo hapo.
 
 Hata hivyo, chanzo cha kifo hicho bado hakijafahamika; maiti imehifadhiwa Hospitali ya Mwananyamala kwa uchunguzi zaidi

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!