ZAIDI ya Wanawake 8,700 hufariki duni kila mwaka nchini Tanzania kutokana na matatizo ya ujauzito na hasa wakati wa kujifungua. Takwimu hizi zinaonesha takribani wanawake 24 hupoteza maisha kila siku huku ikikadiriwa mmoja kufa kila baada ya saa moja.
Hata hivyo wataalamu wa afya wanasema moja kati ya sababu zinazochangia vifo hivi ni kukosekana kwa huduma za dharura katika Vituo vya Afya wakati wa kujifungua. Hata hivyo Serikali ya Tanzania mwaka uliopita katika ahadi zake imeahidi kupunguza vifo hivi kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2015.
“Si sahihi mama mjamzito kufa wakati wa kujifungua au si sahihi mama huyu kupoteza uhai wake kwa kuugawa kwa kiumbe anachokileta duniani, hii haiwezi kukubalika. Na inasikitisha zaidi pale maisha ya mama huyu yanapotea hata kwa mambo ambayo yanaweza kuzuilika,” anasema Rais Kikwete katika hotuba yake mbele ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (U.N) Ban Ki-moon
No comments:
Post a Comment