Pages

Wednesday, 18 September 2013

WATAALAMU WA UMOJA WA MATAIFA WAKIRI KUWA NA USHAHIDI WA MATUMIZI YA SILAHA ZA KEMIKALI KATIKA MAUAJI YA DAMASCUS AGOSTI.



Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wamaliza uchunguzi wao kuhusu matumizi ya silaha za Kemikali

Wataalam wa Umoja wa Mataifa ambao walipewa jukumu la kuchunguza kuhusu matumizi ya silaha za kemikali nchini Syria wamesema katika ripoti yao kwamba kuna ushahidi wa kutosha wa kuwepo matumizi ya silaha hizo aina ya sarin katika mauaji ya Agosti 21 karibu na mji wa Damascus. 

 
Ukurasa wa kwanza wa ripoti, hiyo iliotolewa Jumapili kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ambayo itawasilishwa kuwasilishwa Jumatatu kwa Baraza la Usalama, na kuongeza kuwa silaha za kemikali zilitumika kwa kiwango kikubwa wakati wa vita nchini Syria.


Hayo ni wakati mataifa ya Ufaransa, Marekani na Uingereza yakikutana leo Jumatatu jijini Paris kujadili kuhusu rasimu ya azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ili kuweka sawa makubaliano ya Marekani na Urusi juu ya silaha za kemikali za Syria wakati wakati ripoti muhimu ya wakaguzi kwa Umoja wa Mataifa kuhusu mauaji, ya Agosti 21, ikisubiriwa kutolewa.


Rais wa Ufaransa Francois Hollande akiambatana na waziri wake wa mambo ya nje Laurent Fabious, wamewapokea mapema leo asubuhi, mawaziri wa mambo ya nje wa Uingereza William Hague na John Kerry wa Marekani ambao wanajadili kuhusu muswada wa rasimu ambao viongozi wanatarajia kupasisha kabla ya juma hili kumalizika.


Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Laurent Fabious amesema nchi yake itazingatia ripoti ya wakaguzi wa Umoja wa Mataifa kuhusu mauaji ya Damascus inayotarajiwa kutolewa Jumatatu ili kusitisha msimamo wake. Ameyasema hayo wakati alipompokea katika katika Ikulu ya rais ya Quai d'Orsay mwenziye wa Uingereza, na kuungana na waziri wa mambo ya nje wa Uturuki, Ahmet Davutoglu.


Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, ripoti hiyo ya wakaguzi kuhusu matumizi ya silaha za Kemili itahitimisha matumizi ya silaha hizo bila kutaja muhusika wa mauaji ya watu 21 Aout yaliosababisha mauaji ya watu elfu moja na mia tano, kwa mujibu wa Marekani.


Kwa mujibu wa duru za kidiplomasia, serikali ya Paris inapanga kutumia ripoti hiyo ili kupata uunfgwaji mkono kwenye Umoja wa Mataifa, ambapo rais wa Ufaransa Francois Hollande amesema inabidi kuandaa vikwazo iwapo hakutakuwa utekelezwaji wa mkataba na kwamba kuharibu silaha za kemikali ni hatuwa ya kwanza muhimu, lakini sio njia ya kufikia suluhu ya mzozo wa kisiasa nchini Syria.


Ma waziri wa mambo ya nje wa Marekani Johna Kerry na mwenziwe wa Urusi Sergei Lavrov wameafiki kukutana Septemba 28 ili kupanga kalenda ya mkutano wa amani kuhusu Syria.
Urusi inaweza kuunga mkono uingiliaji kijeshi nchini Syria iwapo serikali ya Syria itakiuka makubaliano. Hata hivyo waziri Lavrov amesema Urusi itafanya uchunguzi kuhusu taarifa zote za tuhuma dhidi ya serikali ya Syria

No comments:

Post a Comment