Pages

Wednesday, 18 September 2013

MVUTANO KESI YA VIGOGO WA "UNGA"


Dar es Salaam. Mvutano mkali wa kisheria uliibuka jana Mahakama Kuu baada ya upande wa mashtaka kutaka kuongeza shahidi wakati wa usikilizwaji wa kesi ya dawa za kulevya inayomkabili raia wa Kenya, Mwanaidi Ramadhani Mfundo, maarufu kwa jina la Mama Leila na wenzake saba.
Ubishi mkali ulianza pale Wakili Mwandamizi wa Serikali, Prosper Mwangamila alipowasilisha ombi la kuongeza shahidi kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Eva Mamuya ambaye alizifanyia dawa hizo uchunguzi wa kimaabara.
Mbele ya Jaji Grace Mwakipesile anayesikiliza kesi hiyo, Mwangamila alisema: “Kwa vile kesi hii inahusu dawa za kulevya, tunaomba shahidi huyu aweze kupata nafasi ya kutoa ushahidi wake”.
Mwangamila ambaye anasaidiwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Peter Maugo aliongeza kuwa mashahidi wote watakaofika mahakamani watatoa ushahidi unaohusu dawa alizofunga Mamuya, hivyo lazima awepo mahakamni kwa ajili ya kuzifungua.
Kwa kuzingatia mazingira hayo, wakili huyo aliiomba Mahakama hiyo iahirishe kesi hiyo hadi leo, ili waweze kuwasilisha taarifa ya kumwongeza shahidi huyo katika mashahidi wao, kwa mujibu wa kifungu cha 289 (1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA).

No comments:

Post a Comment