Monday, 9 September 2013

SAKATA LA MADAWA YA KULEVYA STRAIKA SIMBA SC AKAMATWA NA MADAWA...

                                              
Madawa ya kulevya.
Na Mwandishi Wetu

SURA ya Tanzania inazidi kuchafuka katika suala la usafirishaji wa madawa haramu ya kulevya baada ya mshambuliaji wa zamani wa Simba (jina tunalihifadhi kwa sasa), kukamatwa na madawa ya kulevya kwenye uwanja wa ndege.

Mshambuliaji huyo aliyewahi kuichezea Simba mwanzoni mwa miaka ya 2000, amekamatwa na madawa ya kulevya siku tatu zilizopita kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole jijini Addis Ababa, Ethiopia.
Vyombo vya habari vya ethiopia vimetangaza kukamatwa kwa wanamichezo wawili, mmoja akijitambulisha kuwa ni mchezaji wa zamani wa timu ya simba na timu ya Taifa(Taifa Stars).

Taarifa zimeeleza kuwa wachezaji hao walikamatwa baada ya kutua Bole wakitokea Burundi na wote wawili walikuwa na pasi za kitanzania. Huenda waliamua kupiatia Bujumbura, ili kukwepa ukali wa ulinziulioboreshwa kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA) baada ya waziri wa uchukuzi Harrison Mwakyembe kutaka mambo yawe hivyo na kulivalia njuga suala la madawa ya kulevya.

Mwanamichezo mwingine imeelezwa kuwa aliwahi kuwa bondia. Taarifa zimeeleza kuwa mwanasoka huyo wa simba, alikamatwa wakati akipanda ndege kutoka Addis Ababa kwenda Zurich,Uswiss ambako angepanda treni kuelekea Stokholm, halafu Italy anakoishi.

HABARI KWA HISANI YA GPL.
 

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!