Thursday, 12 September 2013

MTOTO WA MIEZI MITATU AOKOTWA SHAMBANI BAADA YA KUTUPWA NA MTU ASIYEJULIKANA..



MTOTO wa kike mwenye umri wa miezi mitatu ameokotwa katika shamba la mama Feodesia Paulo (37) wakati mama huyo alipofika shambani kwake kwa ajili ya kufanya shughuli zake za kilimo.

Tukio hilo limetokea Ijumaa iliyopita kilomita sita kutoka Mji wa Kahama na kuwashtua wakazi wa mji huo.

Mara baada ya kumuona mtoto huyo, ambaye ametupwa na mtu asiyejulikana, mama Feodesia alimpeleka kwa viongozi wa serikali ya mtaa ambao walimwandikia barua kwenda kwa afisa wa kata.

Afisa wa kata, alimwandikia barua mama huyo na kumtaka ampeleke mtoto huyo kituo cha polisi.

Mkuu wa Kituo cha Kahama, OCD, Ernest Hawii amekiri kumpokea mtoto huyo na kusema kwamba uchunguzi unaendelea.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!