Jumuiya ya Watanzania Sweden, (Tanzaniska Riksförbundet i Sverige), inawakaribisha Watanzania wote hapa Sweden na nchi za Nordic kushiriki kwenye mkutano wa majadiliano ya rasimu ya katiba mpya ya Tanzania utakaofanyika siku ya Jumamosi tarehe 14 Septemba, 2013 kuanzia saa 9 alasiri (15.00hrs) mpaka 12 Jioni (18.00 hrs) kwenye Ubalozi wa Tanzania, Nasby alle 6, 183 55 Taby.
Majadiliano haya yatasimamiwa na kuendeshwa na Professa Francis Matambalya wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambaye kwa sasa yupo Nordic Africa Institute hapa Sweden.
Hii ni fursa maalum na pekee ya kuwasilisha maoni yenu kuhusu rasimu ya katiba mpya na majumuisho ya maoni yenu yatawasilishwa rasmi kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba mapema wiki ijayo.
Wenye nia ya kushiriki kwenye mkutano huu wanaombwa wathibitishe ushiriki wao kupitia anwani ya barua pepe tanzanianswe@hotmail.com au kwa ujumbe mfupi wa simu kwenye namba 0706 50 88 23, au kwa barua pepe:
tanzanianswe@hotmail.com
Karibuni sana!
Katibu /Angela Wilbard
Tanzaniska Riksförbundet Sweden
No comments:
Post a Comment