Saturday, 3 August 2013

MISS AFRICA KUTOKA RWANDA LINAH KEZA AUAWA KWA KUCHOMWA KISU NA MPENZI WAKE HUKO UINGEREZA

         

keza-10
Model kutoka Rwanda aliyewahi kuwa Miss Africa inasemekana ameuawa kwa kuchomwa kisu baada ya kutokea ugomvi kati yake na mpenzi wake wa zamani ambaye pia ni mzazi mwenzake.
Kwa mujibu wa taarifa ya Daily mail, Linah Keza alikutwa amekufa nyumbani kwake mashariki mwa London, Uingereza mbele ya mwanae wa miaka mitatu Jumatano (July 31).
keza-5
Baada ya tukio hilo mpenzi wa zamani wa Linah ambaye anafahamika kama promota aitwaye David Kikawa, 38 alitiwa mbaroni baada ya kujipeleka mwenyewe kituo cha polisi kwa kuhisiwa kufanya mauaji hayo.
keza-7
Marafiki wa karibu na majirani wamesema kumekuwa na ugomvi wa mara kwa mara kwa miezi mingi kati ya wapenzi hao ambao wamekuwa wakiachana na kurudiana mara kadhaa.

Endelea kusoma habari hii kwa kubofya hapa chini



keza-8

Shuhuda mmoja alisema “Nilikuwa nje ndipo nikasikia mtu akipiga kelele na mayowe ndipo nikaamua kukimbia mpaka mlangoni. Mwanamke huyo alikuwa akisema, “vunja mlango uingie”, baada ya kufanya hivyo nikakutana uso kwa uso na mwanaume huyo”.

Baada ya shuhuda huyo kufanikiwa kuingia ndani alimkuta Miss Keza akiwa amelala chini damu zikiwa zimetapakaa huku mtoto wake mwenye miaka mitatu ‘Holly’ akilia pembeni ya mama yake huku David akiwa amesimama na kujaribu kutaka kumshambulia shuhuda huyo kisha akakimbia. Majirani waliwapigia simu polisi majira ya saa 10 na nusu alfajiri ya Jumatano.


keza-9
Holly (mtoto wa Keza)


Binamu wa Linah aitwaye Herbert Muhire aishiye Rwanda amesema David ndiye baba wa mtoto wao na walianza uhusiano miaka 4 iliyopita na waliishi pamoja kabla ya kuachana miezi michache iliyopita.
“Having a child together meant they were in close contact and she wanted to make up and get married, but he was jealous and possessive and would tell her not to see anyone and not to greet anyone and not to go to partie”, aslisema Muhire.
Kwa sasa mtoto wa Lina yuko chini ya uangalizi wa ‘local authorities’ wakati taratibu za kusafirisha mwili wa marehemu kwenda Rwanda zikiwa zinafanywa

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!