Mtoto huyu mchanga anaitwa Aisha aliletwa kituo cha kulelea watoto yatima na kupokelewa na mkuu wa kituo hicho Bi Saida Hassan kwa jina la hapo mtaani watu upenda kumwita Bi Khadija.
Mtoto huyu aliletwa baada ya mama yake mzazi kufariki na, napia bibi yake alifariki na baada ya hapo baba yake na Aisha aliparalaizi mpaka kupelekea kichanga hicho kutopata msaada wowote. Ila Bi Khadija aliamua kumchukua mtoto huyo na kuanza kumlea mpaka tulipomtembelea kituoni hapo tukiwa pamoja na Baadhi ya wasanii wa mziki wa kizazi kipya na Bongo Movie.
Kwa yeyote aliyeguswa ampigie simu Bi Khadija kwa simu ya mkonono ambayo ni
0754584926 na pia kama unataka kufika kituo hiki cha Chawamama kipo Sinza Mori, Jijini Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment