Saturday, 3 August 2013

BAADA YA KUFIWA NIMEIBAINI NAPENDWA!. KHADIJA KOPA

Na Hamida Hassan

MALKIA wa Mipasho Afrika Mashariki, Khadija Kopa amesema baada ya kufiwa na mumewe kipenzi, Jafari Ally, amegundua kuwa anapendwa na watu wengi tofauti na alivyokuwa akifikiria.
Akistorisha na mwandishi wetu, Khadija alisema kuwa kipindi alipokuwa kwenye matatizo alishangazwa na ukaribu ulioonyweshwa na watu hata ambao hakuwatarajia na ameijua nafasi yake kwenye jamii.

 “Nimesaidiwa na asasi mbalimbali, vikundi pamoja na watu wengi, huku wengine wakiniambia kuwa nikitaka msaada niwapigie ingawa sijafanya hivyo, nimefarijika sana kuona napenda kiasi hiki,” alisema mwanamama huyo ambaye anatarajia kumaliza eda Oktoba 16, mwaka huu

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!