Tukio hilo lililovuta hisia za watu wengi limetoea majira ya mchana ambapo Bw. Mrutu alikuwa na gari lake namba T. 508 Ady akielekea magereji na kuvamia gafla na majambazi kwa kumiminiwa risasi muda mfupi baada ya kushuka.
Wekisimulia tukio hilo baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wamemwelezea marehemu kuwa alikutwa na mauti baada ya kujibizana na watu hao waliofika na pikipiki huku wakiulizana masuala yaliyowafanya kana kwamba wanafamiana na kisha kuchukua begi lake muda mfupi baada ya kummiminia risasi tatu kifuani.
Aidha upande wa mafundi gereji ambao walitaka kuficha majina yao walieleza kumzoea afisa huyo kwa kutengeneza magari yake eneo hilo ambapo hufika na maofisa wenzake kama ilivyokuwa leo ambao walitangulia kufika gereji na kutoweka baada ya tukio hilo huku mwenyekiti wa kamati ya ulinzi wa magereji hayo Muntazi Khan akieleza wasiwasi wa tukio hilo kuhusishwa na mgogoro wa magereji hayo na mwekezaji.
Kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi Kinondoni jijini Dar es Salaam Bw. Camilius Wambura aliyewahi kufika katika eneo la tukio kuungana na makachero wa jeshi hilo pamoja na kuomba ushirikiano wa walioshuhudia tukio hilo alikiri marehemu kuwa mtumishi wa serikali na kuahidi kuchukua hatua za haraka na kubaini wahusika na kuwafikisha katika vyombo vya sheria
No comments:
Post a Comment